- Usemi halisi
- Urudiaji
- Sauti igizi
- Matumizi ya viashiria
- Matumizi ya wakati
- Uigizaji
Usemi halisi
Msimulizi anasema moja kwa moja hadhira waweze kuelewa kwa urahisi na wasichoke kusikiliza.
Urudiaji
Kama vipengele vingi vinavyorudiwa kama vile maneno, vifungu, nyimbo n.k.
Sauti igizi
Msimulizi anaweza kuiga sauti fulani kwa kutumia lugha inayomwezesha kubadilisha sauti yake katika fani mbalimbali.
Matumizi ya viashiria
Mtambaji hodari ana ufundi wa kutumia viashiria mbalimbali kukoleza usimulizi wake. Viashiria hivyo ni kama:
- Mikono
- Mikunjo ya uso
- Mchezesho wa macho
- Viungo vingine vya mwili
Matumizi ya wakati uliopo
Wakati uliopo kihistoria au uliopita kisimulizi. Usimulizi huwa katika wakati uliopita lakini pia huchanganya sifa zinazohusisha wakati uliopo ilikuonesha umbali uliopo kati ya hadhira na simulizi umepunguzwa.
Uigizaji
Msimulizi wa hadithi anaiga sauti mbalimbali za wahusika au wanyama katika utambaji wake.